21 Oktoba 2017 - 18:08
 Majeshi ya Syria yakomboa mji wa Alqaryatain

Televishen ya serikali ya Syria imetangaza kuwa majeshi ya Syria yamefanikiwa kuukomboa mji wa Alqaryatain baada ya mashambulizi makali dhidi ya magaidi wa Daesh na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi hao

Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: vyombo vya habari vya Syria vimetangaza habari ya kuwa majeshi ya nchi hiyo yakishiriana na washirika wake kuwa wamekomboa mji wa Alqaryatain uliopo katika mkoa wa Homs nchini Syria.
Aidha televishen hiyo imetangaza kuwa majeshi hayo yameukomboa mkoa huo baada ya kuwaangamiza magaidi wa Daesh walikuwa wakiumiliki mji huo.
Mwanzoni mwa mwezi huu wawakilishi wa taasisi ya kimataifa ya haki za binadamu nchini Syria wametangaza kuwa kikundi cha kigaidi cha Daesh katika shambulio lake dhidi ya majeshi ya Syria wamefanikiwa kuuteka mji wa Alqaryatain.
Wawakilishi hao siku ya Jumamosi aidha wametangaza kuwa kufuatia mashambulizi makali baina ya majeshi ya Syria na magaidi wa Daesh, baadhi ya magaidi wa Daesh wamejisalimisha kwa majeshi ya Syria na wengine wamekimbia mji wa Aqaryatain, huku wakisisitiza kuwa hivi kikundi cha kigaidi cha Daesh baada ya kukimbia katika mji huo, wanamiliki sehemu ndogo ya jangwa iliopo mashariki mwa mkoa wa Homs nchini Syria.
Mji wa Alqaryatain uko na umbali wa kilometa 100 na kufika katika Mji wa kale wa Palmyara na umbali wa kilometa 300 kufika katika mji wa Deir ez-Zor ambapo kwa sasa ndio mapambano makali yanaendelea baina katika ya magaidi wa Daesh na majeshi ya serikali ya Syria.
mwisho/290